MSN YA BARCELONA YAFIKISHA GOLI 100 BARCELONA IKISHINDA 4

Baada ya jana Cristiano Ronaldo kufunga bao 4 katika ushindi wa bao 7-1 walioupata Real Madrid leo Messi amepiga bao 2 kati ya bao 4 walizoshinda Barcelona dhidi ya Eibar




Munir El Haddad alitangulia kufunga kwa upande wa Barcelona kabla ya Messi kufunga bao la pili na kufanya mchezo huo mapumziko Barcelona wakiongoza kwa bao hizo 2-0.

Kipindi cha Pili Vinara hao wa ligi KUU nchini Spain waliongeza bao la tatu kupiria kwa Messi tena safari hii akifunga kwa njia ya penati kisha Luis Suarez akifunga bao la nne na kuwapa Barcelona pointi 3 muhimu

Umoja wa safu ya ushambuliaji ya Barcelona maarufu kama MSN amefikisha magoli 100 msimu huu ukiwa ni ushindi wa 11 mfululizo katika la Liga wakiongeza nafasi ya kutwaa tena kombe msimu huu

No comments

Powered by Blogger.