MBWANA SAMATTA APIGA BAO PEKEE TAIFA STARS IKIIADHIBU CHAD KWAO

Nahodha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta ameibuka shujaa leo huko D'jamena Nchini Chad baada ya kufunga bao pekee katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika.
Samatta akishangilia bao alilofunga leo (picha kutoka BinZubeir)
Samatta anayekipiga katika klabu ya Genk ya Ubelgiji alifunga bao hilo pekee dakika ya 30 ya mchezo huo uliopigwa majira ya SAA 10 za Chad huku kukiwa na joto kali Kipindi hiki.

Samatta alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi ya Farid  Mussa na kuwalamba chenga mabeki wa Chad na kuweka mpira kimiani.

Stars ambayo iko Kundi G inakamata sasa nafasi ya 3 ikiwa na pointi 4 baada ya kucheza mechi 3 wakati Misri wanaoongoza wakiwa na pointi 6 baada ya mechi 2 huku Nigeria wao wakishika nafasi ya pili wakiwa na ponti sawa na Taifa Stars wakati Chad wanashika mkia wakiwa hawana pointi mpaka sasa.

Mechi ya marudiano itachezwa Dar es Salaam Jumatatu ya pasaka.


1 comment:

Powered by Blogger.