REAL MADRID WAMGEUKIA COURTOIS WA CHELSEA KAMA WAKIMKOSA DE GEA
Klabu ya Real Madrid imemweka kipa namba moja wa Chelsea Thibaut Courtois katika orodha ya juu ya makipa wanaotarajiwa kusajiliwa na klabu hiyo kama watamkosa David De Gea wa Manchester United.
Tayari Florentino Perez ameweka nguvu zake kuhakikisha kipa mwenye kiwango cha juu anasajiliwa na klabu hiyo kuweza kumsaidia Kipa wa sasa Keylon Nevas na kipa namba moja anayetajwa ni David De Gea wa Manchester United ambaye ilibaki kidogo asajiliwe na Real Madrid lakini kama akikosekana basi Courtois atachukua nafasi yake.
Kuna kila hali msimu ujao Chelsea watakosa kushiriki michuano ya Ulaya hali ambayo inaweza kupelekea Nyota wengi wanaolipwa mishahara mikubwa kuuzwa ili kuendana na Sheria ya matumizi ya fedha katika Soka na pengine hilo linawapa Real Madrid mwanya wa kuweza kujipanga kumpata kipa huyo ambaye msimu uliopita alikua akiitumikia Atletico Madrid kwa mkopo wa miaka mitatu.
Itakua ngumu Chelsea kumzuia kipa huyo kutimkia Real Madrid kama watakosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya na kipa huyo tayari ameshazoea mazingira ya Jiji la Madrid na hata mpenzi wake ni Mspaniola wa jiji la Madrid.

No comments