MATA ALIMWA KADI NYEKUNDU MAN UNITED IKICHAPWA NA WEST BROMWICH.

Kiungo Mshambuliaji Juan Mata alipata kadi nyekundu katika mechi ambayo Manchester United ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa West Bromwich Albion.



Wakicheza katika dimba La Hawthorn United iliwatumia wachezaji wengi ambao walikua majeruhi akiwemo walinzi Chriss Smalling na Mateo Darmian badala ya kikosi cha vijana ambacho kilitumiwa na timu hiyo katika mechi zilizopita na kupata ushindi dhidi ya Arsenal na Watford katika ligi kuu.

Goli pekee La Wenyeji West Bromwich likifungwa na Mshambuliaji wake Jose Salomon Randon Gimenez aliyetumia vyema pasi ya Mlinzi Sebastian Pocognoli ambaye alikua ameingia dakika chache kabla ya goli hilo.

Kwa matokeo hayo Manchester United wamebaki katika nafasi ya 6 wakiwa na pointi zao 47 huku West Bromwich wakipanda mpaka nafasi ya 11 wakiwa na pointi 39.

No comments

Powered by Blogger.