Taarifa za kuumia kwa kiungo wa Leicester City Ngolo Kante ambaye ataikosa michezo miwili ya timu yake dhidi kuanzia mchezo wa leo dhidi ya West Bromwich Albion na mchezo unaofuata katika ligi kuu nchini England zimepokelewa kwa maono tofauti na Wapenda Soka duniani wengi wakiamini kwamba sasa lile anguko la Leicester City ndilo limefika.
 |
Andy King |
Lakini hali ni tofauti kwa kocha mkuu wa timu hiyo Claudio Ranieri kwani ameshathibitisha kwamba Nafasi ya N'golo Kante itajazwa na mchezaji Andy King ambaye hana wasiwasi nae na anaamini kwamba huu ni wakati wake mkongwe huyu kuonekana.
 |
King - kushoto |
Andy King ndiye mchezaji aliyedumu na Leicester City kwa kipindi kirefu zaidi tangu alipojiunga na klabu hiyo inayotumia uwanja wa King Power mwaka 2004.
Kante ambaye amekua ndiye mhimili wa mafanikio ya Leicester City msimu huu alitolewa katika mechi iliyopita dhidi ya Norwich ambapo Leicester City iliibuka na ushindi wa bao 1-0 akisumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja.
 |
N'golo Kante - kulia |
Leicester City wanaoongoza ligi hiyo leo watakua nyumbani kuwakaribisha West Bromwich Albion katika mchezo ambao watu wengi wanataka kuona kama Leicester City bila N'golo Kante inawezekana na macho yote yatakuwa kwa ANDY KING
No comments