EUROPA LEAGUE YAMRUDISHA KLOPP DORTMUND

Aliyekua kocha mkuu wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp atalazimika kurudi katika dimba la Signal Induna Park kusaka nafasi ya kuivusha Liverpool ambayo anaifundisha hiving sasa katika hatua ya Robo fainali katika michuano ya Europa League.
Liverpool klabu pekee iliyosalia katika michuano hiyo baada ya kuitoa Manchester United katika hatua ya 16 bora imepangwa kucheza na wababe hao wa Bundesliga wanaokamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ya Ujerumani ambao waliitoa Tottenham katika hatua iliyopigwa.

Mabingwa watetezi Savilla wamepangwa kukutana na ndugu zao Athletic Bilbao zote  za Spain hizi huku Villareal ikipangwa kukutana na Sparta Praha wakati Braga ya Ureno itakutana na Shaktar  Donetsk

Mechi hizo zinatarajia kupigwa Alhamisi ya April 7 na marudiano ni April 14.

No comments

Powered by Blogger.