CHELSEA HOI KWA PSG YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA ULAYA

Mabingwa wa England Chelsea jana waliaga rasmi katika mashindano ya mechi za klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuchapwa bao 2-1 na PSG ambao ni Mabingwa wa Ufaransa.




PSG waliingia katika dimba La Stamford Bridge wakiwa tayari na faida ya goli 2-1 walizopata katika mechi za awali katika dimba La Parc de Prince na jana walihitaji Sare tu waweze kutinga hatua ya Robo fainali huku Chelsea wakiwa na mtihani mgumu wa kupata ushindi wa bao 2-0.

Adrien Rabiot Provost alitangulia kuifunga PSG bao la kwanza dakika ya 16 tu ya mchezo akitumia pasi ya Zlatan Ibrahimovic lakini Diego Costa alieisawazishia Chelsea kwa kufunga bao dakika 10 baadae na Zlatan Ibrahimovic akafunga bao la ushindi la PSG dakika ya 67.

Katika mechi nyingine hiyo jana wenyeji Zenit St Petersburg walikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Benfica ya Ureno na kutupwa nje ya michuano hiyo kwa ushindi wa Jumla wa bao 3-1.

No comments

Powered by Blogger.