BBC YA REAL MADRID YARUDI KWA KISHINDO,YAIKANDAMIZA SEVILLA 4
Kurejea kwa Mshambuliaji Karim Benzema kumerudisha ule muungano wa safu ya ushambuliaji ya Real Madrid inayojulikana kama BBC (Bale,Benzema na Cristiano) na jana wakicheza kwa mara ya kwanza pamoja waliisambaratisha Sevilla bao 4-0.
Baada ya Gareth Bale kurejea dimbani jana ilikua ZAMU ya Benzema na wote pamoja na Ronaldo wakifunga bao moja kila mmoja huku goli la tatu la Real Madrid likitengenezwa na Nyota hao wote kwani mpira ulianzia kwa Cristiano Ronaldo akampa Benzema naye akamtangulizia Bale aliyeweka kambani. Bao lingine likifungwa na Jese.
Ushindi huo wa bao 4 ni neema kwa kocha Zinedine Zidane kuelekea katika mchezo wa El Clasico weekend ijayo pia umepunguza wigo wa pointi na Barcelona ambao jana walitoka Sare na Villareal huku Atletico Madrid wakipoteza mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Gijón.
Tumekuwekea hapa highlights za mchezo huo kama hukupata muda wa kuutazama

No comments