YANGA YATANGULIA ROBO FAINALI KOMBE LA FA TANZANIA
Mabingwa wa Tanzania bara YANGA SC imetinga hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation baada ya kuifunga JKT Mlale mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mlale JKT pamoja na ugeni wao ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Shaaban Mgandila dakika ya 21 akin tumia vyema mpira wa krosi maridadi ya Edward Songo na kuwaduwaza Yanga ambao bado wana furaha ya ushindi wa wikiendi dhidi ya Simba.
Mabingwa hao walifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake, Paul Nonga dakika ya 38 aliyemalizia pasi ya winga Godfrey Mwashiuya na bao la mwisho na la ushindi likifungwa na Thaban Kamusoko

No comments