MBINU YA PELLEGRIN YAFANIKISHA MAN CITY KUPATA USHINDI MKUBWA UGENINI, ATLETICO MADRID YABANWA
Mbinu ya kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ya kuwapumzisha mastaa wake katika kipigo cha bao 5-1 walichokipata Manchester City dhidi ya Chelsea mwishoni mwa wiki katika kombe la FA kimeisaidia Manchester City kuibuka na ushindi mnono katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
City Ikicheza ugenini dhidi ya Dynamo Kiev ya Ukraine iliweza kuibuka na ushindi wa bao 3-1 huku Pellegrini alianzisha wachezaji 10 ambao hawakucheza katika mechi dhidi ya Chelsea Jumamosi.
Yaya Toure, David Silva na Sergio Aguero walifunga kila mmoja bao moja katika ushindi huo wa Manchester City na kuiweka City katika hatua nzuri ya kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ambapo sasa itahitajika sare tu iweze kupita katika mchezo wa marudiano jijini Manchester wiki mbili zijazo
Katika mechi nyingine Atletico Madrid wakicheza ugenini walilazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji PSV Eindhoven ya Uholanzi

No comments