YAMEMKUTA GARY NEVILLE APIGWA 7 NA BARCELONA, SUAREZ ATUPIA BAO 4 (+VIDEO HIGHLIGHTS)

Usiku wa jana ulikua mgumu kwa gwiji wa zamani wa Manchester United na England Gary Neville baada ya kuchabangwa bao 7-0 akiwa kama kocha mkuu wa Valencia.



Mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Mfalme ulipigwa katika dimba la Nou Camp ulishuhudia Luis Suarez akifunga bao 4 katika bao hizo 7 huku Lionel Messi akifunga bao 3

Matokeo haya ni mabaya sana kwa Gary Neville ambaye hajafanya vizuri tangu afike klabuni hapo na sasa atahitaji ushindi wa bao 8-0 katika mchezo wa marudiano ili kutinga fainali

Kama Hukuangalia mechi hii, bonyeza kwenye video hapa chini kuionea magoli yote ya mechi hii

No comments

Powered by Blogger.