PISHA NJIA, LEICESTER CITY YAIANGAMIZA VIBAYA MAN CITY KWAO

Vinara wa ligi kuu nchini England Klabu ya Leicester City imezidi kuonyesha kuwa wanastahili kuwa mabingwa wa ligi hiyo baada ya kuendeleza vichapo na safari hii wakiibamiza timu ngumu ya Manchester  City




Leicester City ambao walisafiri mpaka katika jiji la Manchester wameibuka na ushindi mnono wa bao 3-1 dhidi ya Manchester City wanaokamata nafasi ya pili.

Robert Huth alitangulia kufunga bao la mapema kabisa kwa Leicester City akiunganisha mpira uliopigwa toka pombeni ya uwanja.

Mpaka mapumziko Leicester City walikua mbele kwa Bao hilo moja na kurudi kipindi cha pili wakiwa na nguvu na ari zaidi na kufanikiwa kupata bao zingine mbili kupitia kwa Mahrez na Huth tena huku Man City wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Sergio Kun Aguero.

Kwa matokeo hayo Leicester City wamefikisha pointi 53 katika nafasi ya kwanza huku City wakibaki na pointi zao 47 katika nafasi ya pili.

No comments

Powered by Blogger.