EPL ~ LIVERPOOL SARE, SOUTHAMPTON,EVERTON NA NEWCASTLE USHINDI, SPURS YAPAA NAFASI YA PILI

Hatua ya 25 ya ligi kuu ya soka nchini England iliendelea jana jioni baada ya kushuhudia mchezo wa awali Mchana wakati Manchester City wakichapwa nyumbani na vinara Leicester City.




Liverpool wao walikua nyumbani kuwaalika Sunderland ambao wanasuasua katika msimamo wa ligi hiyo na mechi hiyo kumalizika kwa sare ya bao 2-2 Liverpool wakikubali magoli mawili waliyofunga awali kurudishwa.

Southampton wakiwa nyumbani waliifunga West Ham United bao 1-0 goli pekee la dakika ya 6 ya Maya Yoshida katika mchezo ambao Victor Wanyama kwa kadi nyekundu.

Everton wakicheza ugenini waliifunga Stoke City bao 3-0 magoli ya Lukaku, Aaron Lenon na Seamus Coleman

Tottenham Hotspurs wao wakicheza nyumbani waliifunga Watford bao 1-0 shujaa wa mchezo huo akiwa ni Delle Alli ambaye aliingia dakika ya 61 na kutoa pasi ya goli lililofungwa na Kieran Tripper

Kwa matokeo ya mechi za jana Leicester City wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 53 wakifatiwa  na Tottenham Hotspurs wenye pointi 48

MATOKEO YA MECHI ZA JANA JUMAMOSI 06/02/2016 EPL


No comments

Powered by Blogger.