LIGI KUU TANZANIA BARA :JKT RUVU Vs YANGA SC - TATHIMINI


 Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya soka Tanzania Bara Yanga leo jioni watakua katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kumenyana na JKT Ruvu katika mechi ya hatua ya 18 ya ligi hiyo




Yanga itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na jeraha la kuambulia pointi moja katika mechi mbili zilizopita wakipoteza dhidi ya Coastal Union na baadae kutoka sare na Prisons jijini Mbeya.

JKT Ruvu wao hali yao ni mbaya kwani wataingia katika mchezo wa leo wakiwa kama Yanga yani wakiambulia pointi moja katika mechi mbili zilizopita wakitoka sare na Maji Maji kabla ya kutandikwa na Mbeya City.

Katika mechi ya mwisho kukutana baina ya timu hizo Yanga waliifunga JKT kwa bao 4-1

UNACHOPASWA KUKIJUA KUHUSU MECHI HIYO

Yanga wanakamata Usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 40 wakati JKT Ruvu wao wanakamata nafasi ya 14 wakiwa na pointi 13

Yanga imeshinda mara 12 ikatoka sare mara 4 na kufungwa mara moja tu wakati Kagera Sugar wao katika michezo 17 waliyocheza wameshinda mara 3 wakitoka sare mara 4 na kufungwa mara 10

RATIBA YA MECHI ZA LEO VPL

  • Yanga SC vs JKT Ruvu
  • Kagera Sugar Vs Simba SC
  • Azam FC Vs Mwadui FC
  • Maji Maji FC Vs Mgambo 
  • Mbeya City Vs Prisons
  • Ndanda FC Vs Mtibwa Sugar
  • Toto Africans Vs. Coastal Union

No comments

Powered by Blogger.