HUYU NDIYE RAIS MPYA WA SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI

 Anaitwa Gianni Infantino mwenye miaka 45 ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Soka duniani FIFA akimrithi Sepp Blatter ambaye amefungiwa kujihusisha na maswala yote yahusuyo soka kutokana na kukumbwa na kashfa ya Ufisadi katika chombo hicho chenye mamlaka ya juu kabisa katika soka duniani.

Infantino si mgeni machoni pa Wapenda Soka baada ya kujulikana sana wakati akilitumikia shirikisho la soka barani Ulaya  UEFA kama Katibu Mkuu na mara nyingi alikua akionekana wakati wa hafla mbalimbali hususani upangaji wa makundi ya Ligi ya mabingwa  barani Ulaya.
Infantino ameshinda nafasi hiyo  ya Rais wa FIFA jana huko Zurich Uswis akiwabwaga Wagombea wengine ambao ni Rais wa Shirikisho la Soka la Asia, Sheikh Salman  bin Ibrahim  Al-Khalifa, Jerome Champagne wa France na Prince Ali Bin Al Hussein wa Jordan. Huku Mgombea mwingine kutoka barani Afrika  raia wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale yeye alijiengua kabla Kura hazijapigwa.

Katika Uchaguzi huo ambao ilibidi kurudia mara mbili ili kumpata mshindi, Infantino alipata Kura 88 na Salman 85 katika awamu ya kwanza na kulazimisha kufanyika kwa Raundi ya Pili ya upigaji Kura kwa vile idadi inayotakiwa ya kuwa na Kura zaidi ya Theluthi 3 haikufikiwa ambayo Mshindi alitakiwa kuwa na Kura zaidi ya 104.
Katika Raundi ya Pili ya upigaji Kura, Infantino alizoa Kura 115 dhidi ya 88 za Salman na kutangazwa Rasmi kuwa Rais wa FIFA hadi mwaka 2019.

ORODHA YA MARAISI WA FIFA 

1904-06: Robert Guerin (France)
1906-18: Daniel Woolfall (England)
1918-21: no president in place following Woolfall's death
1921-54: Jules Rimet (France)
1954-55: Rodolphe Seeldrayer (Belgium)
1955-61: Arthur Drewry (England)
1961-74: Sir Stanley Rous (England)
1974-98: Joao Havelange (Brazil)
1998-2015: Sepp Blatter (Switzerland)
2016-: Gianni Infantino (Switzerland)

No comments

Powered by Blogger.