EUROPA LEAGUE - MAN UNITED, VALENCIA, LEVERKUSEN NA SPURS ZAPATA USHINDI MNONO

Hatua ya 32 bora ya mechi za michuano ya kombe la Europa league ilihitimishwa usiku wa jana baada ya mechi 15 za mzunguko huo kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya.




Manchester United Ikicheza katika dimba lake la Old Trafford iliibugiza bila huruma klabu ya Midtjyland ya Denmark kwa bao 5-1  katika mchezo ambao Midtjylland wakihitaji sare tu kuvuka hatua hii baada ya kushinda katika mechi ya kwanza kwa bao 2-1.

Magoli ya Man United usiku wa jana yaliwekwa kambani na kinda kutoka Academy yya Man United Marcus Rashford aliyefunga bao mbili, huku Ander Herrera na Memphis Depay wakifunga bao moja kila mmoja wakati kulikuwa pia na goli la kujifunga la mlinzi wa Midtjylland Nicolay Bodurov huku Midtjylland wakitangulia kufunga kupitia kwa Pione Sisto

Katika mechi nyingine nchini Ujerumani wenyeji Bayer Leverkusen waliifunga Sporting Lisbon a Ureno kwa bao 3-1 Magoli ya  Bellarabi  aliyefunga magoli mawili na Calhanoglu aliyefungal bao moja.

Jijini Liverpool wenyeji Liverpool wamesonga hatua inayofata baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 goli la penati ya James Milner

Tottenham wakiwa nyumbani White Hart Lane waliibamiza Fiorentina toka Italia b so 3-0 magoli ya Ryan Mason, Erik Lamela na goli la kujifunga la mlinzi wa Fiorentina Rodriguez.

Gary Neville akiwa na kikosi cha Valencia aliibuka na ushindi wa bao 4-0 na hivyo kufanikiwa kushinda kwa ujumla magoli 10-0  baada ya kushinda katika mechi ya awali bao 6-0

Droo ya upangaji wa ratiba ya hatua ya 16 ya michuano hiyo itafanikiwa leo nchini Ufaransa ambapo tutajua timu  ipi itakutana na ipi katika michuano hiyo

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA 


  • Lokomotiv Moscow 1-1 Fenerbahce 
  • Athletic Bilbao 1-1 Marseille 
  • Bayer Leverkusen 3-1 sporting Lisbon 
  • FC Krasnodar 0-3 Sparta Prague 
  • Lazio 3-1 Galatasaray 
  • Liverpool 1-0 Ausburg 
  • Rapid Wien 0-4 Valencia 
  • Schalke 04 0-3 Shaktar Donetsk 
  • Basel 2-1 Saint-Etienne 
  • FC Porto 0-1 Borussia Dortmund 
  • Manchester United 5-1 Midtjylland 
  • Molde 1-0  Sevilla 
  • Olympiacos 1-2 Anderlecht 
  • SSC Napoli 1-1 Villareal 
  • Tottenham Hotspurs 3-0 Fiorentina 


~ SOKA LETU | JAMII YETU 


No comments

Powered by Blogger.