EUROPA LEAGUE : MAN UNITED KUWAVAA LIVERPOOL, TOTTENHAM WANA MTIHANI MZITO KWA DORTMUND
Ratiba ya michuano ya kombe la Europa league hatua ya 16 bora Imepangwa leo na kushuhudia mechi kadhaa za kuvutia zikipagwa hatua hii.
Manchester United ambao hawajawahi kushinda ubingwa wa Europa league watakua na kibarua kigumu kuikabili Liverpool. United imetinga hatua hii baada ya kuivurumusha nje Midtjylland ya Denmark kwa jumla ya bao 6-3 wakati Liverpool wao waliitupa njema Ausburg ya Ujerumani kwa jumla ya bao 1-0.
Tottenham walio katika kiwango bora hivi sasa wamepangwa kucheza na Borussia Dortmund ya Ujerumani. Tottenham iliiondosha Fiorentina ya Italia kwa jumla ya bao 4-1 wakati Dortmund wakiiondosha mabingwa wa zamani wa Ulaya FC Porto ya Ureno kwa jumla ya bao 3-0.
Gary Neville akiwa na kikosi cha Valencia amepangwa kukutana na Athletico Bilbao katika hatua hii ya 16 bora. Valencia wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mkubwa kabisa wa jumla wa bao 10-0 katika hatua iliyopita wakiifunga Rapid Wien huku Athletic Bilbao wao wakiiondosha Olympic Marseille kwa ushindi wa jumla wa bao 2-1.

RATIBA KAMILI YA HATUA YA 16 BORA IKO HIVI
- Shakhtar Donetsk vs Anderlecht
- Basel vs Sevilla
- Villarreal vs Bayer Leverkusen
- Athletic Bilbao vs Valencia
- Liverpool vs Manchester United
- Sparta Prague vs Lazio
- Borussia Dortmund vs Tottenham
- Fenerbahce vs Braga
Ratiba inaonyesha mechi za awali zitachezwa Alhamis ya Tarehe 10 March na marudiano ni tarehe 17 March 2016. Timu ya kwanza kuandikwa katika ratiba hiyo hapo juu itaanzia mechi zake nyumbani.
~ SOKA LETU | JAMII YETU
No comments