MAN UNITED YAIKANYAGA DERBY COUNTY MARA 3 KOMBE LA FA

Mechi  za Hatua ya nne ya michuano ya kombe la FA nchini England  zilianza jana kwa Manchester United  kuibuka na ushindi  wa bao  3-1  wakiifunga timu ya daraja  la kwanza ya Derby County.




Wayne Rooney  alitangulia kufunga  dakika ya 16  ya mchezo akipokea pasi ya Anthony Martial na kufunga bao lake la 243 kwa klabu hiyo.

George Thorne aliisawazishia  Derby  kwa kufunga bao safi lililodumu  mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili Man United ilicharuka  na kuongeza mashambulizi  wakimtumia  zaidi Anthony Martial na kufanikiwa kupata bao mbili zikifungwa  na Daley Blind na Juan Mata

Kwa matokeo  hayo  Man United  inatinga  hatua ya Tano ya michuano hiyo yenye historia kubwa kwa soka la England


No comments

Powered by Blogger.