BUNDESLIGA IMERUDI LEO NI HAMBURGER SV vs BAYERN MUNICH
Baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka hatimaye ligi kuu nchini Ujerumani imerudi tena kumalizia ngwe ya mwisho huku zikiwa zimeshachezwa mechi 17.
Bayern Munich watakua ugenini kuivaa Hamburger SV katika mechi itakayopigwa muda mchache ujao kwenye dimba la Imtech jijini Hamburg nchini Ujerumani.
Katika mechi ya awali baina ya timu hizo Bayern iliibuka na ushindi wa bao 5-0 nyumbani. Leo itaingia katika pambano hilo ikiwa katika nafasi ya kwanza wakati Hamburger wao wanaoshika nafasi ya 10.
Bayern itawakosa Rafinha, Mario Gotze, Frank Ribery na Medhi Benatia ambao bado wako majeruhi
No comments