VAN GAAL YAMEMFIKA HAPAA, APOTEZA MECHI INAYOWEZA KUMFUKUZISHA MAN UNITED.


Mambo yamezidi kwenda Kombo kwa kocha Luis Van Gaal katika kikosi cha Manchester United baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Norwich City katika pambano la ligi kuu nchini England.




Pambano hilo lililopigwa katika dimba la Old Trafford lilishuhudia Man United ikicheza mpira wa kawaida sana na kushindwa kutengeneza nafasi za mabao huku Norwich wao wakicheza kwa tahadhari kubwa na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Norwich walipata magoli yao kupitia kwa Cameron Jerome na Alexander Tettey wakati goli la United likifungwa na Antony Martial.

Kwa matokeo hayo Man United imetoka nje ya Top 4 hali inayozidisha presha kwa Kocha Luis Van Gaal na Wapenda Soka wengi wametabiri anaweza akafukuzwa kabla ya mwaka mpya.

No comments

Powered by Blogger.