EPL - LEICESTER YAKOMAA KILELENI, CHELSEA YAZINDUKA MAN UNITED YACHAPWA

Jumla ya magoli 22 yamefungwa katika mechi 7 za ligi kuu nchini England jana.




 Vinara wa ligi kuu nchini England klabu ya Leicester City imeendelea kung'ng'ania usukani wa ligi hiyo baada ya kuifunga Everton bao 3-2 mchezo uliopigwa katika dimba la Goodson Park jijini Liverpool

Magoli mawili ya Riyad Mahrez na moja la Shinji Okazaki yalitosha kuwa ushindi muhimu vinara hao wa ligi kuu ugenini.

Katika dimba la Stamford Bridge Chelsea baada ya kumtimua Kocha Jose Mourinho walipata ushindi wa bao 3-1 wakiifunga Sunderland katika mechi iliyoshuhudia Osacar akifunga mabao mawili na bao lingine likifungwa na Pedro

Jijini Manchester Mambo yamezidi kuwa magumu kwa kocha Luis Van Gaal baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Norwich Jerome na Tettey wakiongoza mashambulizi kwa upande wa Norwich wakati Antony Martial akifunga bao la kufutia machozi la United.

Southampton ikiwa nyumbani ilikubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa Tottenham Hotspurs. Dede Alli na Hary Kane walifunga magoli ya Spurs ambayo yamewarudisha top 4.

Crystal Palace wakiwa ugenini dhidi ya Stoke City walizoa pointi 3 muhimu za kuwaweka katika pointi sawa na Tottenham wanaokamata nafasi ya nne na Man United wanaokamata nafasi ya 5.

Palace walishinda bao 2-1  shukrani kwa magoli ya Conor Wickam na Chung- Yong Lee

AFC Bournemouth wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Man United wiki iliyopita jana iliifunga West Brom bao 2-1 ugenini.

Newcastle united walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Aston Villa katika pambano la mwisho siku ya jana.

No comments

Powered by Blogger.