TOTTENHAM NA STOKE CITY ZAZIDI KUPAA LIGI KUU YA ENGLAND


Falsafa za kocha Maurcio Pochettino kuijenga timu bora inazidi kuzaa matunda msimu huu kwa kikosi cha tottenham kuendelea kuimarika kadri siku zinavyozidi kusonga.

Ikiwa ugenini Tottenham iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 wakiifunga Watford katika mechi kali 5 za ligi hiyo zilizoanza majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Magoli ya Spurs yamewekwa kimiani na Eric Lamela na Mkorea Son Hueng-min wakati Watford wakipta bao lao moja kupitia kwa Straika wake Mnigeria Odion Ighalo aliyefunga bao lake la 30 mwaka huu 2015 likiwa pia bao la 14 katika msimu huu.

Katika mechi nyingine Stoke City wakiwa ugenini wameinyuka Everton bao 4-3.
Crystal Palace wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Swansea City ambao mpaka sasa hawana kocha.

Aston Villa wamezidi kushushwa chini baada ya kulambishwa bao 2-0 na Norwich City.
Newcastle wakaambulia kichapo cha bao 1-0 toka kwa West Brom

No comments

Powered by Blogger.