LEICESTER CITY VS MAN CTY: HAKUNA MBABE (VIDEO + PICHA)

Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa King Power, Klabu ya Leicester City imeshindwa kuendeleza rekodi yake ya kufunga goli kwa michezo 14 iliyopita kwa kutoka sare ya bila kufungana pale walipoikaribisha Manchester City.


Mchezo ulianza kwa kasi sana na Man City walianza kulisakama lango la wapinzani wao huku juhudi za Rahim Sterling, Sergio Aguero na Kevin De Bruyne zikishindwa kuleta japo walifanikiwa kufika langoni mwa wapinzani wao

Leicester City wao kipindi cha kwanza walicheza kwa kujilinda sana na mashambulizi ya kushitukiza na kipindi cha pili walijaribu kuvunja ukuta wa Man City lakini juhudi za Mahrez na Vardy hazikuzaa matunda, Huku kazi nzuri ikifanywa na Golikipa wa Leicester City Kasper Schmeichel kwa kuokoa michomo mingi ya Man City

Mchezo umeiacha Leicester City katika nafasi ya Pili huku ikifungana na Arsenal kwa Pointi 39 lakini Arsenal anafaida kubwa ya tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Man City wao wamepanda nafasi moja hadi nafasi ya tatu wakiwa wamejikusanyia alama 36 baada ya kucheza michezo 19 ya Ligi.

Kama hujaona mchezo huo nimekuwekea hapa chini video ya mchezo huo

No comments

Powered by Blogger.