RYAN GIGGS "KUMKIMBIA" VAN GAAL MAN UNITED, SWANSEA WAMGONGEA HODI
Mkongwe na kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs amehusishwa katika orodha ya wanaotajwa kuchukua nafasi ya kuwa kocha mkuu wa Swansea City
Gary Monk aliyekua kocha mkuu wa Swansea alitimuliwa juzi kufatia mfululizo wa matokeo mabaya ambapo katika mechi 11 ameshinda mechi moja tu
Giggs yumo katika orodha ya makocha kadhaa wanaotajwa kuchukua nafasi hiyo akiwemo David Moyes na Brendan Rodgers ambaye aliwahi kuifunza klabu hiyo kutoka Wales huku Giggs akipewa nafasi kubwa.
Giggs anaweza asiwe mzoefu lakini amekuwa Masaidizi wa Meneja wa Manchester United Louis van Gaal na David Moyes msimu wa 2013/2014.
Giggs anatajwa kama mtu anayeweza kuchukua mikoba ya Loius Van Gaal kama Man United watataka kupata kocha wa kuchukua nafasi hiyo mwenye Utamaduni wa klabu hiyo lakini pia uwezekano wa Giggs kuondoka upo pia kwani anaonekana haaminiki na Wales ni nyumbani kwake.
No comments