LEICESTER CITY YAZIDI KUKIMBIZA ENGLAND YAZOA TUZO ZOTE NOVEMBA
Mwaka 2015 unazidi kuwa wa neema kwa vinara wa Ligi Kuu nchini England Leicester City baada ya kuzoa tuzo zote za mchezaji bora na kocha bora wa mwezi Novemba.
Wakati wakiongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 32 wakiwa juu ya wakongwe na wenye historia nzuri katika ligi kuu nchini England kocha wa timu hiyo Claudio Ranieri amechaguliwa kuwa kocha Bora huku Straika wake Jamie Vardy akichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Novemba.
Ndani ya Mwezi Novemba, Vardy, mwenye Miaka 28, alifunga Bao katika Mechi zao zote 3 za Ligi na kuweka Rekodi ya kufunga goli katika Mechi 11 mfululizo za Ligi.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Vardy kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England baada ya kuitwaa pia kwa Mwezi Oktoba.
ORODHA YA WACHEZAJI WALIOSHINDA TUZO HIYO MSIMU HUU
- August: Andre Ayew (Swansea City)
- September: Anthony Martial (Man United)
- October: Jamie Vardy (Leicester City)
- November: Jamie Vardy (Leicester City)
Kwa upande wa kocha bora Claudio Ranieri ametwaa tuzo hiyo akiwa ameiongoza Leicester City kutwaa Pointi 7 kati ya 9 kwa Mwezi Novemba kwa kuzifunga Watford bao 2-1, Newcastle bao 3-0 na kutoka Sare ya bao 1-1 na Man United.
No comments