"TEAM LONDON" ZAFUZU KISHUJAA LIGI YA MABINGWA ULAYA NI ARSENAL NA CHELSEA
Mabingwa wa kombe la FA Arsenal na mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England klabu ya Chelsea usiku wa kuamkia leo zimetinga hatua ya 16 bora kishujaa baada ya kupata ushindi katika mechi zao.
Arsenal walihitaji kufunga magoli zaidi ya mawili na wasiruhusu goli lolote ugenini walipoivaa Olympiakos ya Ugiriki na vijana hao wa Arsene Wenger waliweza kuibuka na ushindi wa bao 3-0
Shujaa wa Arsenal jana alikua Olivier Giroud baada ya kufunga mabao matatu peke yake katika pambano hilo lililoshuhudiwa na watazamaji 31388 katika dimba la Karaiskaki.
Jijini London Chelsea wakisahau matokeo mabovu katika ligi waliibamiza FC Porto ya Ureno kwa bao 2-0. Goli la kujifunga la Ivan Marcano na goli zuri la Willian yalitosha kupunguza presha kwa kocha Jose Mourinho ambaye majaliwa yake hayajajulikana baada ya mwenendo mbaya katika ligi.

No comments