LIGI KUU BARA : SIMBA NA AZAM USIOMBE KUHADITHIWA, YANGA KUJILIPUA KWA MGAMBO?



Baada ya kusimama kwa wiki kadhaa kupisha mechi za timu ya Taifa katika michunao ya kufuzu kwa kombe la Dunia navile michuano ya Challenge, Ligi kuu ya Soka ya Vodacom Tanzania bara itaendelea leo kwa mechi kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti.



Jijini Dar es Salaam pambano linalotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka ni baina ya mabingwa wa Afrika mashariki na kati klabu ya Azam FC watakaoivaa Simba katika mchezo utakaopigwa katika dimba la Taifa.

Azam wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 25 huku Simba ikishika nafasi ya nne na pointi zao 21 zote zikiwa zimeshacheza mechi 9 . Simba itaingia katika pambano la leo ikiwa na sura mpya kadhaa wakati Azam wao kikosi chao kikiwa hakina mabadiliko.

Jijini Tanga mabingwa watetezi Yanga watakua wageni wa Mgambo JKT katika pambano ambalo linatajwa kuwa gumu kwa mabingwa hao watetezi kwani Mgambo wamekua imara sana wanapocheza katika uwanja wa nyumbani.

RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO


  • Azam FC vs Simba SC
  • Mgambo JKT vs Yanga SC
  • Kagera Sugar vs Ndanda FC
  • Mbeya City vs Mtibwa Sugar
  • Majimaji FC vs Toto Africans

No comments

Powered by Blogger.