LA LIGA : REAL MADRID YACHAPWA, ATLETICO MADRID YASHINDA NA VALENCIA YA GARY NEVILLE YANUSURIKA KICHAPO.
Real Madrid jana walikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Villareal na kuifanya kubaki na pointi 5 nyuma ya wanaoongoza Barcelona na wanaokamata nafasi ya pili Atletico Madrid.
Villareal ambao ndiyo walikua wenyeji wa mchezo huo walifunga bao la mapema kufatia makosa ya kiungo Luka Modric na mpira kumpata Cedric Bakambu ambaye alimtengenezea Roberto
Soldado nabkuupitisha mpira miguuni pa kipa Keylor Navas.
Katika mechi nyingine siku ya Jana Athletico Madrid waliweza kuiangamiza Athletico Bilbao kwa kuifunga bao 2-1 magoli ya Atletico Madrid yakifungwa na Saul Niguez na Griezman ambaye alifunga bao la umbali wa mita zaidi ya 25 huku Bilbao wao wakitangulia kufunga kwa bao la mshambuliaji Aymeric Laporte.
Ugenini katika uwanja wa Eibar wenyeji Eibar waliweza kuikamata Valencia na kulazimisha sare ya bao 1-1 ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kocha Gary Neville katika La Liga.
Eibar wakitangulia kupata bao kupitia kwa Sergi Enrich kabla ya beki wa Eibar David Junca hajajifunga na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mechi ya mapema kabisa hiyo Jana Rayo Vallecano walikubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Malaga.

No comments