EPL ~ ARSENAL YARUDI KILELENI, NEWCASTLE YAISHUSHA CHELSEA MPAKA NAFASI YA 16.

Kikosi cha kocha Arsene Wenger kimeendeleza kutoa dozi kwa kuifunga Aston Villa bao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini England pambano lililopigwa katika dimba la Villa Park jijini Birmigham jioni ya jana.



Arsenal ilipata magoli yake kupitia kwa Olivier Giroud aliyefunga kwa njia ya penati na lingine likifungwa na Aaron Ramsey na kuwafanya mabingwa hao wa kombe la FA kushika usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 33 huku Aston Villa wakibaki mkiani mwa ligi hiyo wakiwa na pointi 6 tu mpaka sasa.
Katika pambano lingine Newcastle wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kuwafunga Tottenham bao 2-1 katika uwanja wa nyumbani wa Tottenham White Hart Lane jijini London.

Magoli mawili ya Aleksandar Mitrovic na Ayoze Perez huku Tottenham wakitangulia kupata bao kupitia kwa Eric Dier yaliweza kumaliza pambano hilo kwa ushindi kwa vijana hao wa kocha McLaren

Kwa matokeo hayo ni kama kusema Newcastle Imeibeba Man United kwa kulinda nafasi ya nne kwani kama Newcastle ingefungwa basi United walikua wakitoka katika top 4 huku kukiwa na bahati mbaya kwani kwa ushindi huo Chelsea wameshuka mpaka nafasi ya 16 wakiwa na pointi moja juu ya timu zinazoweza kushuka daraja.

Jijini Liverpool Majogoo wa jiji wametoka sare ya bao 2-2 na West Bromwich Albion Magoli ya Liverpool yakifungwa na Jordan Henderson na Divock Origi huku West Brom wakipata mabao yao kupitia kwa Craig Dawson na Jonas Olsson.

Ligi hiyo itaendelea tena leo Jumatatu kwa Vinara wa ligi hiyo Leicester City kukipiga na mabingwa watetezi Chelsea

No comments

Powered by Blogger.