BAO LA DAKIKA YA MWISHO LAIPA YANGA USHINDI MUHIMU TANGA

Bao la dakika ya 95 la kiungo Thabani Kamussoko limeipa Yanga ushindi muhimu katika pambano la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya African Sports ya Tanga.




Pambano hilo lililopigwa katika dimba la Mkwakwani lilishuhudia timu ya African Sports ikicheza kwa umakini mkubwa na kutoruhusu washambuliaji wa Yanga kutumia nafasi walizokua wakitafuta.

Dakika 5 za mwamuzi ndizo zilizoinyima African Sports kupata japo pointi moja huku makosa ya kipa wa African Sports kuutema mpira wa krosi wa Beki wa Yanga Mwinyi Haji na kumkuta Donald Ngoma ambaye alimtengenezea Kamusoko naye kufunga kwa shuti hafifu.

No comments

Powered by Blogger.