UGANDA YATANGULIA NUSU FAINALI CHALLENGE YAIZAMISHA MALAWI
Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda maarufu kama Uganda The Cranes kimeizamisha timu ya taifa ya Malawi kwa kuichapa bao 2-0 katika mchezo wa Kwanza wa Robo fainali ya mashindano ya kombe la Challenge uliomalizika mchana huu huko nchini Ethiopia.
Uganda inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga Ya Tanzania Milutin Sredojevic Maarufu kama Micho imesheheni wachezaji wengi wanaocheza katika ligi ya Uganda ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa Farouk Miya dakika ya 5 tu baada ya kuanza kwa pambano hilo. Goli ambalo lilidumu mpaka mapumziko
Kipindi cha pili kilipoanza tu iliwachukua Uganda kuandika bao la pili na safari hii likifungwa na Ceasor Okhuti na kuwafanya Uganda ambao walikua na kasi katika mchezo huo kumaliza wakiwa na ushindi huo wa bao 2-0 hivyo kuwafanya kuwa ndiyo timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali huku Kilimanjaro Stars ikiingia katika Mechi yake ya Robo fainali jioni hii dhidi ya wenyeji Ethiopia.

No comments