SAMATA NDANI YA KUMI BORA ZA WANAOWANIA UCHEZAJI BORA AFRICA



Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika Klabu ya TP Mazembe, Mbwana Ally Samata amefanikiwa kuingia katika orodha ya wachezaji kumi wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani

Samata amefanikiwa kuingia hatua hii akitokea kwenye orodha ya mwanzo iliyokuwa na wachezaji 24 iliyotolewa mapema mwezi wa kumi.

Image result for samataKatika orodha hii mpya yenye wachezaji 10 Samata atakuwa akichuana na wachezaji wenzake waTP Mazembe ambao ni Robert Kidiaba, Roger Assale'. Wachezaji wengine na kwenye mabano ni Klabu wanazochezea ni Abdeladim Khadrouf (Moghreb Tetouan, Morocco), Baghdâd Bounedjah (Etoile du Sahel, Tunisia), Felipe Ovono (Orlando Pirates, South Africa)

Wengine ni pamoja na Kermit Erasmus (Orlando Pirates, South Africa), .Mohamed Meftah (USMA, Algeria), .Moudather el Tahir (AL HILAL, Sudan) na Zein Edin Farahat (USMA, Algeria)

Samata anatarajiwa kuiongoza timu yake ya TP Mazembe katika fainali ya pili dhidi ya USMA ya Algeria, mchezo huo utakaokuwa marudiano utapigwa nyumbani kwa TP Mazembe ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa Algeria, TP Mazembe iliibuka na ushindi wa goli 2 ambapo Samata Alifungwa Goli la ushindi kwa njia ya penati.


No comments

Powered by Blogger.