KOCHA MPYA ASTON VILLA AKARIBISHWA NA KICHAPO
Masaa machache baada ya kuteuliwa kuwa kocha Mkuu wa Aston Villa Remi Garde alishuhudia timu yake ikifungwa bao 3-1 na Tottenham katika uwanja wa White Hart Lane jijini London.
Tottenham walianza kupata mabao mawili kupitia kwa Moussa Dembele na Delle Alli kabla ya Jordan Ayew kufunga bao moja ambalo liliwarudisha Villa katika mchezo lakini Harry Kane alipoteza kabisa matumaini ya Villa kwa kufunga bao la tatu.
Kwa matokeo hayo Aston Villa wamebaki katika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 4 baada ya michezo 11 huku Spurs wakipanda mpaka nafasi ya 5.
No comments