MATOKEO YA MECHI ZA LEO EPL: MAN CTY YARUDI KILELENI, VARDY WA LEICESTER AWEKA REKODI (VIDEO)

Kipute cha ligi yenye hamasa kubwa Ulimwenguni, Ligi kuu ya Uingereza (EPL) leo kimeendelea tena kwa mechi kadhaa katika viwanja mbalimbali  vya Uingereza. Man City walikuwa nyumbani Etihad na wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 3 dhidi ya 1 la Southampton. Kwa Ushindi huo Man Cty wamefanikiwa kurudi keleleni kwa point 29 huku wakiongoza kwa tofauti kubwa ya magoli ya kufanga na kufungwa.



Leicester Cty ambao wamekuwa na mwanzo mzuri wa Ligi, wamfanikiwa kupata pointi 1 mbele ya Man UTD na kuweza kujikusanyia jumla ya pointi 29 sawa na Man Cty ila wao wakiwa na idadi ndogo ya magoli. Kivutio kikubwa katika mchezo huo ilikuwa ni Kwa Mshambuliaji wao "Jamie Vardy" ambapo dunia ilikuwa inasubiri kama ataweza kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeweza kufunga katika mechi 11 mfululizo za Ligi ya Uingereza hasa baada ya kufikia rekodi ya Van Nestrooy ya kufunga mechi 10 mfululuzo hapo wiki iliyopita.

Vardy alihitaji dakika 24 tu kuweza kuweka rekodi yake baada ya kufunga goli katika dakika hiyo lilioipa Leicester Cty nafasi ya kuongoza kabla ya Man UTD kusawazisha dakika 45.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa leo ni kama ifuatavyo:
  • AFC Bournemouth 3 – 3 Everton
  • Aston Villa 2 – 3 Watford
  • Crystal Palace 5 – 1 Newcastle United
  • Manchester City 3 – 1 Southampton
  • Sunderland 2 – 0 Stoke City
  • Leicester City 1 – 1 Manchester United

Video ya magoli ya Leicester City  Vs Man United



Video Ya Magoli ya mechi ya Man Cty vs Southampton

No comments

Powered by Blogger.