MAJANGA: KILIMANJARO STARS YATUPWA NJE KOMBE LA CHALLENGE

Uwakilishi wa Tanzania katika kombe la Challenge mwaka huu umehitimishwa kwa timu ya Taifa ya Tanzania bara kutolewa na Ethiopia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3.




Mchezo huo wa Robo fainali ya pili ulichezwa katika uwanja wa taifa wa soka ulioko Adiss Ababa ulishuhudia Killi Stars wakitandaza soka la uhakika huku wakiwashambulia Ethiopia mara kwa mara kupitia kwa washambuliaji John Bocco, Malimi Busungu,Said Juma Ndemla na Simon Msuva.

John Bocco ambaye ni nahodha wa kikosi hicho alitangulia kuipatia Stars bao la kuongoza dakika ya 25 kabla ya Gatoch Panom ambaye pia ni nahodha wa Ethiopia hajaisawazishia timu yake kwa mkwaju wa penati na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ndipo mwamuzi alipoamuru kupigwa mikwaju ya penati.

Katika mikwaju hiyo Kilimanjaro Stars ilikosa penati mbili huku Ethiopia ikipata penati 4 zote ambazo walikua wamepiga. Waliokosa Penati kwa upande wa Stars walikua Ni Jonas Mkude na Shomari Kapombe wakati John Bocco, Hassan Kessy na Himid Mao ndiyo waliopata penati zao.

No comments

Powered by Blogger.