BALLON D'OR 2015: NI MESSI, RONALDO NA NEYMAR

Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar Jr ndiyo wamefanikiwa kuingia tatu bora ya wachezaji wanaowania Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2015. Kwa miaka kadhaa sasa Ronaldo na Messi ndiyo wamekuwa wakipokezana kuchukua Tuzo hiyo kubwa kwa upande wa wachezaji huku Messi akibeba mara nne mfululizo na Ronaldo akibeba mara tatu.


Neymar ambaye alikuwa na msimu mzuri huku magoli yake yakiisaidia Barcelona kuchukua Ubingwa wa La Liga, Kombe la Mfalme na Klabu Bingwa Ulaya hii imekuwa ni mara yake ya kwanza.

Tuzo hiyo ya Ballon D'OR itatolewa Januari 11, 2016 pamoja na tuzo za Kocha bora wa Mwaka, mchezaji bora wa mwaka (kwa upande wa wanawake), Timu bora ya mpira wa miguu (FIFApro), Goli bora la mwaka.

Majina ya washiriki na vipengele walivyoingia ni kama ifuatavyo:


FIFA Ballon d'Or:
  • Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal), Lionel Messi (Barcelona/Argentina), Neymar (Barcelona/Brazil).

Mchezaji Bora wa Mwaka (Wanawake):
  • Carli Lloyd (Houston Dash/USA), Aya Miyama (Okayama Yunogo Belle/Japan), Célia Šašić (FFC Frankfurt/Germany)
Kocha Bora wa Mwaka (Wanaume)

  • Pep Guardiola (Bayern Munich), Luis Enrique Martínez (Barcelona), Jorge Sampaoli (Chile).

Kocha Bora wa Mwaka (Wanawake)
  • Jill Ellis (USA), Mark Sampson (England), Norio Sasaki (Japan).

Goli Bora la Mwaka
  • Alessandro Florenzi (Roma v Barcelona, 16/09/15), Wendell Lira (Atletico-GO v Goianesia, 11/03/15), Lionel Messi (Barcelona v Athletic Bilbao, 30/05/15).
Kama hukufanikiwa kuyaona magoli haya nilishakuwekea HAPA

No comments

Powered by Blogger.