LIGI YA MABINGWA ULAYA - MAN CITY KATIKA MTIHANI MZITO NA JUVENTUS, MAN UNITED KUIKARIBISHA PSV

Mechi 8 zinatarajiwa kuchezwa leo katika mzunguko wa 5 wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mechi za makundi A,B,C na D kuchezwa katika viwanja tofauti barani humo.



Baada ya kujeruhiwa katika El Clasico Real Madrid watakua ugenini kuwakabili Shaktar Donetsk wakati PSG wao watakua ugenini kumenyana na Malmo katika mechi za Kundi A.

Manchester United itakua nyumbani Old Trafford kuikaribisha PSV Eindohovein ya Uholanzi huku CSKA Moscow watakua nyumbani kuwakaribisha VFL Wolsfburg ya Ujerumani kukamilisha mechi mbili za kundi B.

Pambano linaloweza kuvuta hisia za mashabiki wa soka leo ni lile litakalopigwa Jijini Turin kati ya Juventus na Manchester City mechi ya kundi D

HII NDIYO RATIBA KAMILI YA MECHI ZOTE ZA LEO KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI

KUNDI A
10:45 PM - Malmo FF vs Paris Saint-Germain
10:45 PM - Shakhtar Donetsk vs Real Madrid

KUNDI B
8:00 PM - CSKA Moscow vs VfL Wolfsburg
10:45 PM - Manchester United vs PSV Eindhoven

KUNDI C
6:00 PM - FC Astana vs Benfica
10:45 PM - Atletico Madrid vs Galatasaray

KUNDI D
10:45 PM - Borussia Monchengladbach vs Sevilla FC
10:45 PM - Juventus vs Manchester City

UJUMBE MAALUMU KUTOKA WAPENDA SOKA TANZANIA
... Tarehe 1 January kila mwaka ni siku maalumu ya Wapenda Soka (Wapenda Soka Day) ambapo tunaungana kusaidia watoto yatima kwa chochote kile Mungu alichotujalia kwa mwaka mzima na kuomba baraka zake kwa mwaka mpya.
Ungana nasi basi kuchangia chochote.
Maelezo zaidi na Mawasiliano
0715 127272 - C.E.O
0717 685055 - Katibu
0717 664685 - Mweka Hazina
.. SOKA LETU JAMII YETU

No comments

Powered by Blogger.