BAADA YA KICHAPO SASA KIBARUA CHA BENITEZ MASHAKANI. ZIDANE KUKABIDHIWA TIMU?


  • - Anasubiri huruma ya Florentino Perez kubaki Bernabeu.
  • Wachezaji wamkumbuka Carlo Ancellot





Siku mbili baada ya kupata kichapo cha aibu cha bao 4-0 toka kwa Barcelona katika mechi ya El Clasico, kocha mkuu wa Real Madrid Rafael Benithez huenda akatimuliwa klabuni hapo.

Benitez ambaye ana miezi michache tu tangu alipoteuliwa kuinoa klabu hiyo tajiri duniani anakosolewa si tu kwa kufungwa na Barcelona bali jinsi timu inavyocheza kwa ujumla pamoja na mahusiano yake na wachezaji wa timu hiyo hasa Cristiano Ronaldo.

Jioni hii Rais wa Real Madrid Florentino Perez ameitisha mkutano na waandishi wa habari na Wapenda Soka wametabiri kuwa yawezakuwa ni kuhusu majaliwa ya kocha huyo japokuwa Rais wa Zamani wa Real Madrid Ramon Calderon anaamini kuwa Benitez hatotimuliwa.

Kumekuwa na msuguano mkubwa ndani ya kikosi cha Madrid ikisemekana kuwa wachezaji wengi wanamuunga mkono aliyekua kocha mkuu wa timu hiyo Carlo Ancellot ambaye wanaamini haikuwa sawa kumfukuza.

Nyota wa zamani wa Real Madrid mfaransa Zenedine Zidane ambaye anafundisha kikosi cha vijana cha Madrid anatajwa kwa kiwango kikubwa kumrithi Benitez kama atatimuliwa japo yeye mwenyewe ameanaamini Benitez hawezi kutimuliwa .

Real Madrid inakamata usukana katika kundi lake kwenye ligi ya mabingwa Ulaya wakati katika La Liga wanakamata nafasi ya 3 nyuma ya Barcelona wanaoshika nafasi ya kwanza na Atletico Madrid wanaokamata nafasi ya pili.

No comments

Powered by Blogger.