UWARIDI JK NDANI YA ANFIELD
Muasisi mmoja wa jarida la success magazine la nchini marekani bwana Leonard Cohen aliwahi kusema "there is a crack in everything that's how the lights get in" kauli yake hii ya matumaini kwa sasa wanaishi nayo mashabiki wengi wa timu ya Liverpool kama sio wa soka kwa ujumla baada ya Jurgen Klopp kukabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo yenye makazi yake pale Merseyside...
Tangu kutimuliwa kwa Benitez na kuondoka kwa Alonso, Mascherano na El Ninho dunia imeiona Liverpool ikipitia ktk safari ngumu ya machozi,jasho na dimbwi la damu huku wapenzi wa soka wakijiuliza iko wapi Liverpool iliyoinyanyasa Madrid ulaya au ile United bora kabisa ya hivi karibuni ilivyonyanyasika kwenye ngome yake pale OT,majibu ya maswali haya watu wameyakosa kwa muda mrefu
,..Brendan Rodgers alijaribu kwa namna yake kuirudisha heshima ya Liverpool akiwa na Suarez, Sturridge na Sterling lile soka lake la kushambulia liliendana sawia na hao wachezaji lakini alipowakosa Danny(majeruhi) na Luis(kuuzwa) msimu uliofuata alishindwa kuiaminisha dunia kwamba alikuwa bora bila ya mchawi Suarez na guu la kushoto la Sturridge... alishindwa kuupata ubora wa ndani kwa wachezaji wake aliokuwa nao hapa ndipo unapotoa heshima kwa Wenger na Ferguson wakiwa na vikosi vya kawaida kabisa waliwezaje kupata walivyovitaka hata baada ya kuondokewa na wachezaji wao nyota.
Leo hii Liverpool wanaianza safari na tumaini lao jipya chini ya mjerumani Jurgen Klopp aliyeichezea timu 1 tu maisha yake yote ya soka"Mainz 05" kwa miaka 11 na baadae kuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2001 alipostaafu...wakati anaichukua BvB alisema anapenda soka la mapambano ambalo kila mtu lazima achafuke na wachezaji wanapokwenda majumbani wasiweze kucheza mpira hata kwa majuma manne...huyu ndiye Klopp ambaye aliwahi kumzaba kibao mtangazaji mwenzie wa televisheni moja nchini ujerumani alipomwambia kila mtu anakusifia kwa uamshaji wako wa morali..ningelikuwa mchezaji wako kwa sasa ungenifanya nini..ni katika makocha vijana wanaokuja vizuri sana japo hakumaliza vzuri BvB na Mainz,kwa mbali hapa naliona tabasamu la moyoni la Emre Can anajua hatocheza tena kama CB,Firmino pia anajua atacheza na Coutinho sehemu ambayo atakuwa huru kama alivyofanya kwa Kagawa na Gotze kucheza pamoja.
Natarajia kumuona Carragher sky sports akiizungumzia Liverpool ambayo itatumia gegen pressing na ndio hasa filosofia ya Klopp kuwafanya wapinzani wakose muda wa kukaa na mpira na kufanya maamuzi sahihi ya wapi pa kuupeleka,namuona Koeman mwingine ndani ya Klopp kwa aina ya mchezo wanayocheza na mifumo wanayoitumia kutoka 4-2-3-1 kwenda 4-3-3 au hata 4-3-1-2 kutokana na mahitaji ya mbinu na wapinzani wenyewe kwa wakati huo..vilevile ujio wake waweza kuwa baraka kwa wale wanaotakiwa kuondoka Liverpool au kinyume chake kwa wale ambao ndio wanaonekana kuwa roho ya timu kwa sasa.
Binafsi naamini ataleta mabadiliko ndani ya Liverpool japo siyatarijii msimu huu na nina imani kama ya wamiliki wa Liverpool kuwa ni mtu sahihi kuitoa klabu ilipo kwenda mahala pazuri zaidi na pia nina uhakika zile nafasi nne za juu kuna timu itatoka isipojikaza ukiitoa City...United, Arsenal na Chelsea hizi timu msimu huu zinaunga mno leo wako vizuri kesho wanaharibu ikiwa muorobaini wa Klopp ukifanya kazi haraka kwa mgonjwa Liverpool na hizo timu zikiendelea na viwango vyao kama homa za vipindi tutaongea mengine mwishoni mwa msimu..karibu uwaridi linukialo na soka lako la kasi na mashambulizi ya haraka na kushitukiza ambalo Moreno na Clyne watafaidika nalo mno
Zahir Bilali
0712436593
No comments