MWAKA WA SHETANI : CHELSEA YAPIGWA 3 NA LIVERPOOL DARAJANI.


Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England Klabu ya Chelsea imeendeleza wimbi lake la matokeo mabaya msimu huu baada ya kukubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa Liverpool katika dimba la Stamford Bridge

Mechi hiyo ya Ligi kuu nchini England imeongeza presha kwa kocha Jose Mourinho na Wapenda Soka wengi wanatabiri mwisho wa Mourinho katika Klabu hiyo ambayo ilikua ikimwona kama shujaa wao.

Liverpool ambayo inafundishwa na Juggen Klopp hivi sasa iliweza kupata mabao yake kupitia kwa Philip Countinho ambaye alifunga mabao mawili moja likiwa dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza akisawazisha goli la Chelsea lililofungwa na Ramires.

Benteke ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya James Milner alifunga bao la tatu na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 3-1 matokeo ambayo yanaiacha Chelsea katika nafasi ya 15 huku Liverpool wakipanda mpaka nafasi ya 7 .

VIKOSI
Chelsea (4-2-3-1):
Begovic; Zouma, Cahill, Terry,Azpilicueta (Falcao 75); Ramires, Mikel (Fabregas
69), Willian; Oscar, Hazard (Kenedy 59),Costa

Subs not used: Baba,Remy, Matic, Amelia

Mfungaji: Ramires 4'

Kadi ya njano: Mikel

Liverpool (4-3-3):

Mignolet; Clyne, Skrtel, Sakho,Moreno; Can, Lucas, Milner (Benteke 64); Lallana
(Lovren 90), Coutinho, Firmino (Ibe 75)

Subs not used: Allen, Bogdan, Teixeira, Randall

Wafungaji: Coutinho 45+3, 74, Benteke 83

Kadi za njano: Coutinho, Lucas, Can, Benteke

Watazamaji: 41,577

Refa: Mark Clattenburg

No comments

Powered by Blogger.