MAN UNITED, MAN CITY,CHELSEA NA ARSENAL MAMBO SAFI ENGLAND


Jumla ya magoli 23 yalifungwa katika mechi 8 za ligi kuu nchini England jana ukiwa ni mzunguko wa 9 tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi hiyo inayopendwa na kufatiliwa zaidi duniani.

Vinara wa ligi hiyo Manchester City walikua nyumbani kuwaalika AFC Bournamouth kwa bao 5-1 shukrani kwa Raheem Sterling ambaye alifunga mabao matatu kabla hata ya mapumziko na Wilfried Bony akaongeza mawili kufikia matano.

Majirani zao Manchester United wao walikua ugenini katika uwanja wa Goodson Park jijini Liverpool kuwakabili Everton na Magoli ya Morgan Scheneiderlin, Ander Herrera na Wayne Rooney yalitosha kuwapa ushindi wa bao 3-0 Man United jioni hiyo.

Arsenal wakiwa ugenini wameendeleza makali yao baada ya kuwafunga Watford kwa bao 3-0 magoli ya kipindi cha pili ya Alexis Sanchez, Olivier Giroud na Aaron Ramsey ushindi uliowapeleka Arsenal mpaka nafasi ya pili wakiwa na pointi 19 sawa na Man United wanaokamata nafasi ya 3.

Mabingwa watetezi Chelsea baada ya kuanza vibaya msimu huu walijitutumua na kushinda bao 2-0 nyumbani darajani wakiifunga Aston Villa. Diego Costa alitangulia kufunga bao dakika ya 34 ikiwa ni mechi yake ya kwanza baada ya kutoka katika kifungo cha kufungiwa mechi 3. Bao la pili la Chelsea lilikua ni bao la kujifunga la mlinzi Alan Hutton.

Liverpool wao wakiwa na kocha mpya Juggen Klopp walishindwa kupata ushindi ugenini dhidi ya Tottenham Hotspurs na kuambulia sare ya bila kufungana

Southampton wakiwa nyumbani walilazimishwa sare na Leicester City ya bao 2-2 licha ya Southampton kutangulia kufunga mabao mawili mpaka mapumziko.

Crystal Palace wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa West Ham. West Brom waliitandika Sunderland bao bao 1-0.

No comments

Powered by Blogger.