MAJANGA KWA MOURINHO, ATUPWA NJE CAPITAL ONE CUP HAZARD AKOSA PENATI


Kocha Jose Mourinho amejikuta akizidi kujiweka vibaya na kuhatarisha kazi yake baada ya kutupwa nje katika kombe la Capital One Cup ambalo Chelsea walikua ndiyo mabingwa watetezi.


Chelsea imetupwa nje kwa changamoto ya mikwaju ya penati na Stoke City baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ndipo ikabidi kupigwa penati ambapo Eden Hazard alikosa penati moja huku Stoke wakifunga zote

Jonathan Walters alitangulia kuipatia Stoke bao la kwanza kabla ya Loic Remy kusawazisha dakika za lala salama na ndipo mikwaju ya matuta ikatumika.

No comments

Powered by Blogger.