VODACOM WAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZA VPL
Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu
Tanzania bara leo imekabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo yenye
thamani ya shilingi milioni 490,00,000.
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alisema kuwa kwa mara
nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom
inakidhi vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi,
viatu na vifaa vingine vinayohitajika.
Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo
tukiwaa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu
zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya 2015/2016”
Alisema Twissa.
Twissa alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa
sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi
hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata
buruddaniya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa
duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa
kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka sekta hii.
Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili
kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiri
katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa
kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za
vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi ya chini ambako vinapaswa
kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface
Wambura aliishukuru Kampuni ya Vodacom na kuvitaka vilabu vinavyoshiriki ligi
kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa ligi.
Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo
ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa” alisema.
Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sharia
kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya
madhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na
maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitakazoshiriki zimejiandaa vya
kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.
No comments