NIGERIA KUWASILI LEO USIKU
Timu ya Taifa ya Nigeria
(Super Eagles) inatarajiwa kuwasili leo alhamis saa nne usiku kwenye uwanja wa
JK Nyerere jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege binafsi tayari kwa mchezo
dhidi ya Tanzania siku ya jumamosi uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari
na Mawasiliano cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Nigeria (NFF), kupitia
kwa Toyin Ibitoye msafara huo unatarajiwa kuwa na wachezaji 23 pamoja na
viongozi wa benchi la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu Sunday Oliseh pamoja
na viongozi wengine waandamizi wa shirikisho hilo.
Nigeria inatarajiwa kufanya mazoezi siku ya ijumaa saa 10
jioni katika uwanja wa Taifa, ikiwa ni mazoezi mepesi ya kuelekea kwenye mchezo
huo.
No comments