SIMBA SHANGWE TUPU TANGA, AZAM YAUA CHAMAZI


Mabingwa wa mwaka 2012 Simba ya Dar es Salaam imeanza vizuri mtanange wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuifunga timu ngeni ya African Sports katika pambano la kwanza kwa timu hizo baada ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu leo.

Iliwabidi Simba kusubiri mpaka kipindi cha pili kujipatia goli lao pekee katika mchezo huo likifungwa na mshambuliaji mpya wa timu hiyo toka Uganda Hamis Kiiza "Diego" bao ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Jijini Dar es Salaam mabingwa wa kombe la Afrika mashariki matajiri watengeneza Ice Cream klabu ya Azam FC ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani Azam Complex iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 wakiifunga Prisons ya Mbeya

MATOKEO YOTE YA MECHI ZA LEO LIGI KUU TANZANIA BARA

African Sports 0-1 Simba SC
Azam FC 2-1 Prisons FC
Toto African 1-0 Maadui FC
Ndanda FC 1-1 Mgambo JKT
Majimaji FC 1-0 JKT Ruvu
Mbeya City 0-1 Kagera Sugar
Stand United 0-1 Mtibwa Sugar

No comments

Powered by Blogger.