MAJANGA CHELSEA YAPIGWA 3-1 NA EVERTON, MOURINHO HALI TETE




Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England Chelsea wameendeleza mwanzo mbaya wa ligi msimu huu baada ya kukubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa Everton.

Steven Naismith aliibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga mabao yote matatu na kuifanya Chelsea kupoteza mchezo wa tatu katika michezo mitano waliyocheza tangu kuanza kwa ligi hiyo.

Naismith aliingia dakika ya 9  kuchukua nafasi ya Muhamed Besic aliyeumia na kufunga mabao hayo matatu la kwanza akilifunga dakika ya 17 na dakika nne badae akafunga la pili kabla ya Nemanja Matic kufunga bao la kufutia machozi na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Everton wakiongoza kwa bao 2-1.

Kipindi cha pili ilikua ni kumalizia tu kazi kubwa iliyofanywa kipindi cha kwanza kwa Naismith kufunga bao la tatu dakika ya 83 na kuzidi kuishusha Chelsea katika msimamo na kuhatarisha kibarua cha kocha Jose Mourinho ambaye msimu uliopita alifanya vizuri sana.

MAMBO UNAYOPASWA KUYAFAHAMU BAADA YA KIPIGO HICHO

Matokeo ya kupata pointi 4 katika michezo mitano ambayo Chelsea imezipata mpaka sasa ina maana ni mara ya kwanza kupata matokeo mabovu katika historia ya klabu hiyo tangu mwaka 1986.

Msimu uliopita Wakati Chelsea walipochukua ubingwa walipoteza mechi tatu tu ambazo wameshazipoteza mpaka sasa.

Steven Naismith amekua mchezaji wa kwanza kufunga Hat-trick (magoli matatu au zaidi) katika ligi kuu nchini England dhidi ya timu inayofundishwa na Jose Mourinho.

Naismith amekuw mchezaji wa sita kufunga hat trick akitokea benchi katika mechi za ligi kuu nchini England.

Amekua pia mchezaji wa tano kugunga hat trick katika ligi kuu nchini England dhidi ya Chelsea mara ya mwisho alikua Robin van Persie akiwa na Arsenal mwezi October 2011.

Hii ni mara ya kwanza kocha Jose Mourinho anapoteza mechi mechi mbili mfululizo katika ligi tangu May 2006.

Mara ya mwisho Chelsea walianza msimu vibaya  ilikua msimu wa 1986/87 walipocheza mechi 5 hawakushinda mechi yoyote walitoka sare mara 3 na kupoteza mara 2 na walimaliza msimu huo wakishika nafasi ya 14.

No comments

Powered by Blogger.