MASKINI ADEBAYOR, TOTTENHAM YALIKATA JINA LAKE


Mshambuliaji  Emmanuel Adebayor ameachwa katika orodha ya majina ya wachezaji wa Tottenham Hotspurs katika michuano ya ligi kuu Nchini England na ile ya Europa League ambayo Spurs watashiriki.


Mchezaji huyo Raia wa Togo alijunga na Spurs mwaka 2012 akitokea Manchester City kwa gharama ya paundi milioni 5.

Adebayor mwenye miaka 31 ameathiriwa sana na maswala ya kifamilia yaliyokua yakimkabili ila amefanikiwa kufunga magoli 18 katika mechi 47 tangu aliposainiwa kama mchezaji kamili baada ya kukaa hapo kwa mkopo msimu uliotangulia.

West Ham na Aston Villa ni kati ya klabu zilizoonyesha kumtaka mchezaji huyo ila sakashindwa kutokana na mshahara mkubwa anaolipwa Spurs hivi sasa.


No comments

Powered by Blogger.