MAJANGA ARSENAL, WELBECK NJE YA DIMBA MPAKA CHRISTMAS
Wakati mashabiki wa Arsenal wakijiuliza kwanini kocha wao Arsene Wenger amesajili mchezaji mmoja tu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji, majanga yameanza kujitokeza baada ya mshambuliaji wake Danny Welbeck ambaye ni majeruhi kusemekana atakaa nje ya uwanja mpaka Mwezi wa 12.
Welbeck mwenye miaka 24 amefanyiwa operesheni kubwa ya goti baada ya kuumia mwezi April katika sare ya bila kufungana na Chelsea.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Arsenal msimu uliopita akitokea Manchester United ameshafunga magoli 9 katika mechi 34 alizoichezea Arsenal.
Ni pigo kwa safu ya ushambuliaji ya Arsenal hasa baada ya kumkosa Karim Benzema katika dirisha la usajili lililofungwa juzi hivyo kufanya Arsenal kubaki na Olivier Giroud kama mshambuliaji wa kutegemewa huku wakiwemo Theo Walcott, Alexis Sanchez na Joel Campbell ambao mara nyingi hushambulia wakitokea pembeni.
No comments