CHELSEA,ARSENAL NA AS ROMA WAAMBULIA VICHAPO LIGI YA MABINGWA ULAYA


Hatua ya pili ya mechi za makundi katika ligi ya mabingwa Barani Ulaya ilianza jana kwa Arsenal,Chelsea,As Roma zote zikipata vichapo katika mechi zao.

Roma wakiwa ugenini walilambishwa bao 3-2 na BATE Borisov katika   mechi ya  kundi E  mechi iliyokua kali muda wote.

Barcelona wakachomoza na ushindi wa bao 2-1 nyumbani wakiifunga Bayer Leverkusen katika mechi ambayo Barcelona walipata magoli dakika za mwisho baada ya kutangulia kufungwa katika kundi hilo hilo la E

Katika kundi F Arsenal wakiwa nyumbani walifungwa bao 3-2 na Olympiakos wakati Bayern Munich waliifunga Dianamo Zagreb bao 5-0.

Chelsea walikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa FC Porto ikiwa ni ukaribisho wa kocha Jose Mourinho katika dimba la Dragao watazamaji 46,120 wakishuhudia pambano hilo.

MATOKEO NA WAFUNGAJI MECHI ZOTE ZA JANA

KUNDI E

● BATE Borisov 3-2 As Roma
  - Igor Stasevich (8')
  - Filip Mladenovic (12',31)
  - Gervinho (66')
  - Vasilios Torosidis (82')
 
● Barcelona 2-1 Bayer Leverkusen
  - Papadopoulis (22')
  - Sergi Roberto (80')
  - Luis Suarez (82')

KUNDI F

● Arsenal 2-3 Olympiakos
  - Felipe Padro (33')
  - Theo Walcot (35')
  - David Ospina (40') OG
  - Alexis Sanchez (65')
  - Finnbogason (66')

● Bayern Munich 5-0 Dinamo Zagreb
  - Douglas Costa (13')
  - Roberto Lewandowski (21',28', 55')
  -Mario Goetze (25')

KUNDI G

● Fc Porto 2-1 Chelsea
  - Andre Andre (39')
  - Willian (45')
  - Maicon (52')

● Maccabi Tel Aviv 0-2 Dynamo Kyiv
  - Yarmolenko (4')
  - Junior Moraes (36')

KUNDI H

● Lyon 0-1 Valencia
  - Sofiane Feghouli (42')

● Zenit 2-1 Gent

  - Artem Dzyuba (35')
  - Thomas Matton (56')
  - Oleg Shatov (67')

No comments

Powered by Blogger.