MAN UNITED YATOA KIPIGO CHA NGUVU: ROONEY APIGA HAT TRICK


Nahodha wa Man United Wayne Rooney amefunga mabao matatu katika ushindi wa bao 4-0 walioupata Manchester United dhidi ya Club Brugge katika ligi ya mabingwa barani Ulaya

Wakisafiri mpaka Ubelgiji United waliibuka na ushindi huo katika Mechi hiyo ya marudiano kuwania kupata nafasi ya makundi ya ligi hiyo maarufu duniani

Mpaka mapumziko United ilikua ikiongoza kwa bao 1-0 huku kipindi cha pili wakionekana kubadilika zaidi na kupeleka mashambulizi yaliyozaa magoli mengine matatu Wayne Rooney akifunga mawili na moja la kiungo Ander Herrera.

United sasa imevuka kuingia hatua ya makundi ya ligi hiyo kwa ushindi wa jumla wa bao 7-1 baada ya kushinda katika mechi iliyopita kwa bao 3-1.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA

  • Apoel 1-1 Fc Istana
  • Bayer Leverkusen 3-0 Lazio
  • CSKA Moscow 3-1 Sporting Lisbon
  • Man United 4-0 Club Brugge
  • Partizan Zone 2-1 Bate 




No comments

Powered by Blogger.